Monday, April 1, 2013

ISIPOKUWA MLIAMINI BURE.

1 WAKORINTHO 15:1-2

BASI NDUGU ZANGU NAWAARIFU ILE INJILI NILIYOWAARIFU, AMBAYO NDIYO MLIYOIPOKEA, NA KATIKA HIYO MNASIMAMA, NA KWA HIYO MNAOKOLEWA: IKIWA MNAYASHIKA SANA MANENO NILIYOWAHUBIRI; ISIPOKUWA MLIAMINI BURE.

Neno la Mungu (hapo juu) linatuambia habari ya injili ambayo kwa hiyo tunapokea zawadi au neema ya kuokolewa na kupokea uzima wa milele. Injili ya YESU KRISTO ambayo ndani yake kuna nguvu ya kutuokoa.

Ili upokee wokovu ni lazima uisikie injili ya Yesu Kristo na habari ya Ufalme wa Mungu Baba, pasipo injili ya Yesu Kristo hakuna wokovu, injili ya Yesu Kristo pekee!

Matendo ya mitume 10:3-6.

Kornelio, mtu mtauwa (hajaokoka bado) anatokewa na malaika katika maono, anaambiwa atume mtu kwa Simoni Petro, aje nyumbani mwake amwambie yampasayo kutenda….


Matendo ya mitume 11:14

Malaika yule anamwambia Kornelio amwite Simoni Petro aje amwambie maneno au habari itakayomwokoa… injili ya Yesu Kristo!

Matendo ya mitume 16:30-32

Baada ya milango ya milango ya gereza kufunguka, na mlinzi wa gereza kutaka kujiua Paulo na Sila wakamzuia. Wakamwambia habari njema ya Yesu Kristo… injili ya Yesu Kristo! Wakamwambia mwamini Bwana Yesu nawe utaokoka, wakamwambia neno la Bwana (Yesu), yeye na nyumba yake yote, wakaokoka.

Mathayo 24:14 na Marko 13:10.

Neno la Mungu linazidi kututhibitishia kuwa hakuna wokovu pasipo injili ya Yesu Kristo na Ufalme wa Mungu. Injili inahubiriwa na itahubiriwa ulimwenguni kote ili wewe ambaye bado hujampokea Yesu Kristo na hujaokoka upate nafasi ya kupokea zawadi hiyo.

Baada ya kuisikia injili ya Yesu Kristo na kuokoka ni lazima uishi maisha ya kudumu na kutekeleza kinachokuambia katika injili ya Yesu Kristo. Kuishi maisha tofauti na injili ya wokovu ni kazi bure, ni kupoteza muda. IKIWA UNAISHIKA SANA INJILI ULIYOHUBIRIWA NA UNAYOHUBIRIWA, UTAPOKEA UZIMA WA MILELE.

2 Yohana 1:9

Mungu anakuambia, usipodumu kufuata, kutenda na kuishi mafundisho ya injili ya Yesu Kristo, hauna Mungu. Wokovu ulioupokea, pasipo kuishi ikuelekezavyo injili ya Kristo, ni ubatili mtupu na kujilisha upepo.

Luka 6:46.

Yesu Kristo anakuhoji, kwanini unajiita umeokoka, mkristo, unaimba kwaya, wewe ni kiongozi na unahudhuria ibada lakini hauyatendi anayokuelekeza katika injili yake?

Ikiwa unaisikia na kuisoma injili ya Yesu na hujaokoka bado, ni lazima uamue leo kumpokea Yesu Kristo na uyakabidhi maisha yako kwake, uokoke.

Na ikiwa wewe ni mkristo, lakini unatenda kinyume na injili ya Yesu Kristo, ni lazima ubadilike sasa. Neno la mungu linakuambia, kuishi kinyume na injili ni bure, imani yako ni bure!

                         BONYEZA HAPA: Uokoke.

No comments:

Post a Comment

Featured Post

HAIJALISHI TUNAKOSEA MARA NGAPI? MUNGU NI MUAMINIFU KILA WAKATI

Nakusalimu kupitia Jina kuu lipitalo majina yote, Jina la Yesu Kristo, Bwana na Mwokozi wetu. Mungu wetu ni muaminifu, hajawahi kuse...

Popular Posts