Tuesday, April 28, 2020

HAIJALISHI TUNAKOSEA MARA NGAPI? MUNGU NI MUAMINIFU KILA WAKATI


Nakusalimu kupitia Jina kuu lipitalo majina yote, Jina la Yesu Kristo, Bwana na Mwokozi wetu.

Mungu wetu ni muaminifu, hajawahi kusema uongo (uongo siyo tabia ya Mungu, ni tabia ya ibilisi-shetani kwani yeye ni muongo tangu awali na ni baba wa huo), kamwe hatengui agano lake na siku zote huitazama ahadi yake ili akaitimize. Kila agano na ahadi iliyopo ndani ya neno la Mungu kupitia Biblia takatifu, ni lazima litatimizwa kwa wakati unaofaa.

Wakorintho 10:13
Hakuna jaribu lo lote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Na Mungu ni mwaminifu; hataruhusu mjaribiwe kupita uwezo wenu. Lakini mnapojaribiwa atawapa na njia ya kutokea ili mweze kustahimili.


Yohana 1:9
Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki na atatusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote.



1 Wakorintho 1:9
Mungu ni mwaminifu ambaye aliwaita muwe na ushirika na Mwanae, Yesu Kristo, Bwana wetu.


2 Wathesalonike 3:3
Lakini Bwana ni mwaminifu. Atawaimarisheni na kuwalinda kutokana na yule mwovu.
 


2 Timotheo 2:13
Tusipo kuwa waaminifu, yeye huendelea kuwa mwaminifu kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.


Waebrania 10:23
Tushikilie kwa makini tumaini tunalokiri kwa maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu.




1 Petro 4:19
Basi wale wanaoteswa kufuatana na mapenzi ya Mungu, wajikabidhi kwa Muumba wao aliye mwaminifu.


Kumbukumbu la Torati 7:9
Basi jueni ya kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hadi vizazi elfu.




Zaburi 91:4
Kwa manyoya Yake atakufunika, chini ya mbawa Zake utapata kimbilio; uaminifu Wake ni ngao na kigao.

Mtie moyo mpendwa mwenzako kwa kushiriki naye somo hili. Mungu akubariki sana. Amina.

Featured Post

HAIJALISHI TUNAKOSEA MARA NGAPI? MUNGU NI MUAMINIFU KILA WAKATI

Nakusalimu kupitia Jina kuu lipitalo majina yote, Jina la Yesu Kristo, Bwana na Mwokozi wetu. Mungu wetu ni muaminifu, hajawahi kuse...

Popular Posts