Saturday, October 12, 2013

KWANINI YESU KRISTO ALIPOTAKA KWENDA FARAGHA, KATIKA MAOMBI, AU ALIPOAMUA KUFANYA JAMBO LA KIPEKEE ALICHAGUA KUAMBATANA NA PETRO, YOHANA NA YAKOBO?



 Ukiyachunguza maandiko katika vitabu vya Biblia vya Injili zile nne; Injili ya Mathayo, Marko, Luka na Yohana utakutana na vifungu vingi vikionesha jinsi Bwana wetu Yesu Kristo alivyopenda kuambatana na Petro, Yohana na Yakobo.

Na alipenda kuambata na wanafunzi wake hao watatu; Petro, Yohana na Yakobo sehemu muhimu au katika shughuli muhimu. Kwa mfano, alipotaka kwenda faragha kwa maombi au alipoamua kufanya jambo la uponyaji lililohitaji imani kubwa.

Kuna sababu nyingi sana zilizomfanya Bwana wetu Yesu Kristo apende kuambatana na wanafunzi wake hao watatu katika faragha na sehemu muhimu mbali mbali.

Petro, Yohana na Yakobo richa ya kwamba walikuwa ndugu (Yakobo na Yohana - Mathayo 4:21) na marafiki (Marko 13:3, Matendo ya Mitume 3:1) walikuwa wana sifa za pamoja zinazofana na sifa za kila mmoja wao, ambazo kwa umoja wao walitengeneza timu iliyompendeza Yesu Kristo.

Hebu tuangalie baadhi ya vifungu vinavyo thibitisha kuwa Bwana wetu Yesu Kristo alipenda kuongozana zaidi na Petro, Yohana na Yakobo kwa maombi ya faragha au katika jambo la kipekee na umuhimu zaidi.

Mathayo 17:1. Na baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, akawaleta juu yam lima mrefu faraghani (kwa maombi).

Marko 1:29. Na mara walipotoka katika sinagogi, walifika nyumbani kwa Simoni na Andrea, pamoja na Yakobo na Yohana. Naye mkwewe Simoni, mamaye mkewe, alikuwa kitandani, hawezi homa; na mara wakamwambia (Yesu Kristo) habari zake.  (Yesu Kristo) Akamkaribia, akamwinua kwa kumshika mkono, homa ikamwacha, akawatumikia.

Marko 5:37. Wala hakumruhusu mtu afuatane naye, ila Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye Yakobo.

Luka 22:8. Akawatuma Petro na Yohana, akisema, Nendeni, mkatuandalie pasaka tupate kuila.

Marko 14:32-33. Kisha wakaja mpaka bustani iitwayo Gethsemane, akawaambia wanafunzi wake, Ketini hapa muda niombapo. Akamtwaa Petro na Yakobo na Yohana pamoja naye, akaanza kufadhaika sana na kuhangaika.

Featured Post

HAIJALISHI TUNAKOSEA MARA NGAPI? MUNGU NI MUAMINIFU KILA WAKATI

Nakusalimu kupitia Jina kuu lipitalo majina yote, Jina la Yesu Kristo, Bwana na Mwokozi wetu. Mungu wetu ni muaminifu, hajawahi kuse...

Popular Posts