Thursday, July 4, 2019

SADAKA YA USHAWISHI


Sadaka ni nini?
Sadaka igusayo moyo hutolewa katika upendo (Picha:clipart-library.com)

Sadaka ni toleo la thamani (kwako unayetoa mfano wa fedha, mnyama au mali ya aina nyingine) kwa Mungu kwa makusudi ya kupata baraka, kibali, toba au kutii agizo la Mungu (Mwanzo 22:2, 1 Wafalme 17:13-16 na Mambo ya Walawi 4). Sadaka inagawanyika katika makundi mawili makubwa; 1. Sadaka ya kumwaga damu, sadaka hii ilianzishwa na kumalizwa na Mungu mwenyewe. Baada ya Adam na Eva kumkosea Mungu kwa kula tunda la mti wa katikati, Mungu aliwavika vazi la ngozi ya mnyama, hii maana yake Mungu alimwaga damu ya mnyama ili kuwavika vazi la kuficha dhambi yao (Mwanzo 3:21). Kupitia kumwaga damu kwa Yesu Kristo katika kifo cha msalaba, dhambi za wanadamu zinasamehewa na kufutwa kabisa (Waebrania 9:22, Mathayo 5:17, Yohana 3:16, Matendo ya Mitume 4:12 na Yohana 1:29). 2. Sadaka isiyomwaga damu, sadaka hii ni mazao ya ardhi kama nafaka, matunda n.k. Sadaka inaweza kutolewa moja kwa moja kwenye madhabahu ya Mungu ama ikatolewa kwa mwanadamu mwingine. Mara zote sadaka inayotolewa kwa mwanadamu inapaswa kutolewa kwa wenye uhitaji mfano wajane au yatima wasiojiweza (Yakobo 1:27). Sadaka inatakiwa kutolewa kwa moyo wa kupenda kwa kadiri Roho wa Mungu atakavyosema nawe (kwa kadiri ya sauti ya utoaji utakayoisikia moyoni au nafsini mwako). Sadaka itolewayo kana kwamba unamsaidia Mungu ama unatoa ili mradi uonekane machoni pa watu kuwa nawe umetoa haimbariki Mungu na kamwe usitegemee kuugusa moyo wa Mungu kwa utoaji huo na pia usitegemee Baraka za Mungu (Marko 12:41-44).

Maana ya sadaka ya ushawishi
Sadaka ya ushawishi ni sadaka inayotolewa ili kumshawishi Mungu akutatulie changamoto unayoipitia kwa wakati huo. Aina na kiasi cha sadaka hii hutolewa maelekezo na Mungu mwenyewe, mara nyingi unapokuwa katika maombi ya kuomba mkono wa Mungu ukuokoe kutoka katika shida Fulani ndipo utasikia sauti ya Mungu ikikuelekeza kutoa sadaka ya aina na kiasi fulani katika madhabahu fulani au kumpatia mtu fulani. Siyo kila anaeingia katika maombi ya kuomba msaada wa Mungu ataelekezwa kutoa sadaka hii. Mungu alipotaka kufanya agano na Ibrahimu (baba yetu wa Imani), Ibrahimu alimuuliza Mungu kuhusu uzao na Mungu akamjibu Ibrahimu kuwa atampatia uzao lakini alitaka kwake (kwanza) amtolee sadaka (Mwanzo 15). 

Tofauti ya sadaka ya ushawishi na nadhiri
Sadaka ya ushawishi ni sadaka inayotolewa kwanza (muamini akiwa ndani ya kifungo au shida) ili Mungu afungue milango ya kifungo fulani wakati sadaka ya nadhiri ni sadaka ambayo muamini anaahidi kumtolea Mungu mara baada ya Mungu kumvusha katika kifungo au shida fulani. Kwa mfano, katika hali ya udhaifu au ugonjwa, muamini anamtolea Mungu sadaka inayosukuma maombi yake ili Mungu aachilie uponyaji (hii ni sadaka ya ushawishi) na ahadi ya sadaka anyotoa muamini kumpatia Mungu mara baada ya kuponywa (hii ni sadaka ya nadhiri). 

Wakati gani ni sahihi kutoa sadaka ya ushawishi?
Wakati sahihi wa kutoa sadaka ya ushawishi ni mara baada ya kusikia sauti ya Mungu ikikuelekeza kufanya hivyo. 

Faida za sadaka ya ushawishi
Faida kuu ya sadaka ya ushawishi ni kumuonesha Mungu utii na imani yako kwake na hivyo kumfanya aharakishe katika kuachilia majibu ya maombi yako.

Featured Post

HAIJALISHI TUNAKOSEA MARA NGAPI? MUNGU NI MUAMINIFU KILA WAKATI

Nakusalimu kupitia Jina kuu lipitalo majina yote, Jina la Yesu Kristo, Bwana na Mwokozi wetu. Mungu wetu ni muaminifu, hajawahi kuse...

Popular Posts