Yohana 1:12. “Bali wote
waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio
Jina lake”.
Katika mstari huo juu,
tunajifunza vitu vikubwa viwili kulingana na somo letu. Moja, kufanyika watoto
wa Mungu. Pili, kuliamini Jina la Yesu Kristo au kumuamini Yesu Kristo. Kumbuka
somo letu linasema “kuukulia wokovu na neema ya Mungu”, katika somo la kwanza
tuliona namna ya kumuamini Mungu (Yehova) na Yesu Kristo. Kupitia imani hiyo
ndipo tunapata haki ya wokovu.
Kwa maana hiyo,
tunapoamini na kupata wokovu tunafanywa kuwa wana wa Mungu aliye hai (Yehova).
Kuwa mtoto wa tajiri na
kuwa mtoto wa tajiri na wakati huo huo rafiki wa moyoni ni vitu viwili tofauti
na kuna faida tofauti. Utanielewa baada ya vifungu vifuatavyo vya Biblia.
Isaya 41:8. “Nawe,
Israeli, mtumishi wangu; Yakobo, niliyekuchagua; mzao wa Ibrahimu, rafiki yangu (Mungu)”
Yakobo 2:23.”Maandiko
yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa
ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu”
Katika mstari wa kwanza
tumejifunza kuwa ukimwamini Mungu na Yesu Kristo unafanyika mtoto wa Mungu,
lakini katika mistari miwili ya hapo juu tunaona kuwa kuna watu ambao Mungu
anawaita rafiki zake.
Hata wewe leo hiii
ukiamua kuendelea mbele zaidi na uhusiano wako na Mungu kutoka kuwa mtoto wa
Mungu hadi kufikia kuwa rafiki wa Mungu, INAWEZEKANA, hebu tuangalie mstari
ufuatao kwa uthibitisho;
Yohana 15:14. “Ninyi
mmekuwa rafiki zangu, mkitenda
niwaamuruyo”.
Kwa hiyo katika mstari
huo hapo juu tunaona jinsi Yesu Kristo anavyokiri kuwa kuna watu wanaoweza kuwa
rafiki wa Mungu. Lakini ipo gharama katika kuwa rafiki wa Mungu, gharama hiyo
ni kutenda kila Mungu analokuamuru kulitenda pasipo kuchagua.
Na, kufanyika rafiki wa
dunia ni kufanyika adui wa Mungu. Kutenda kwa kufuatisha namna na mwenendo wa
dunia unaopendeza na kuvutia macho ambao ndani yake kuna udhalimu ni kujifanya
rafiki na dunia. Na kwa njia hiyo (kuwa rafiki wa dunia) tunajiondolea haki na
nafasi ya kuwa rafiki wa Mungu (Yakobo 4:4, Warumi 8:7)
Kuna faida katika kuwa
mtoto na rafiki wa Mungu, kumbuka mfano wangu wa kwanza. Ukiwa mtoto na rafiki
wa Mungu, Mungu hatakuficha kitu (Yohana 15:15).
Kumbuka, Mungu
alipowatuma Malaika kuiharibu miji ya Sodoma na Gomora; wale Malaika walipokelewa
na Ibrahimu na Lutu. Lakini Mungu alimfunulia siri hiyo Ibrahimu kwanza, ni kwa
sababu Ibrahimu alikuwa rafiki wa Mungu (Mwanzo 18:17).
Katika kumalizia somo
letu lenye kichwa “HATUA ZA KUUKULIA WOKOVU NA NEEMA YA MUNGU”, tunamalizia na
HATUA YA KUFANYIKA RAFIKI WA MUNGU.
KUDOWNLOAD PDF YA SOMO
LOTE, BONYEZA HAPA
KUMPOKEA YESU KRISTO
KUWA BWANA NA MWOKOZI WAKO, BONYEZA HAPA