Baada ya Lucifer (ibilisi) kuasi, Mungu na Utatu wake
Mtakatifu waliamua kumfanya/kumuumba mtu kwa mfano wao. Mtu ambaye walimuumba
kwa mfano wao; ambaye ana roho, nafsi na mwili.
Mwanzo 1:26 “Mungu
akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu…”. Katika mstari huo
wa kitabu kitakatifu cha Mungu, Biblia tunaona kuwa Mungu alikuwa akifanya
makubaliano na mtu au watu zaidi ya mmoja juu ya kumuumba mtu au mwanadamu. Na
aliokuwa akifanya nao maamuzi ya uumbaji wa mtu ni nafsi zake mbili, yaani
Mungu mwana (Yesu Kristo) na Mungu Roho Mtakatifu. Mungu katika Utatu wake
Mtakatifu ndiye aliye amua kumuumba mtu au mwanadamu kwa ajili ya utukufu wake,
na mwanadamu huyu aliumbwa kwa makusudi maalumu ya Mungu mwenyewe.
Inaaminika kwamba Lucifer (ibilisi) alikuwa miongoni mwa
malaika wakuu watatu wa Mungu, wengine wakiwa ni Malaika Gabrieli na Malaika
Mikaeli amabaye ni malaika wa vita. Wakati ule Lucifer (ibilisi) alikuwa ni
malaika mkuu wa sifa, ambaye alikuwa akimpa Mungu utukufu kwa jinsi ya maumbile
yake.
Katika ufalme wa Mungu, muundo wa uongozi wa Mungu ulikuwa
hivi; Utatu Mtakatifu wa Mungu ndiyo ulikuwa mkuu ukifuatiwa na Malaika hao
Wakuu watatu (Lucifer, Gabriel na Michael) na hatimaye walifuatia malaika
wengine.
Lakini Lucifer (ibilisi) alipokubali kumuasi Mungu ili
akiinue kiti chake juu zaidi ya kiti cha enzi cha Mungu, akitaka kujipa nafasi
ya Mungu ndipo aliponyang’anywa utukufu aliokuwa nao na kutupwa hadi kuzimu
amabko anatawala jeshi la malaika wao waliokubali kuungana naye katika
kumpindua Mungu. Malaika hao waovu ndiyo wajulikanao kama mapepo hivi leo
kutoka ufalme wa giza ambao idadi yao ilikuwa ni theluthi ya malaika
waliokuwepo Mbinguni wakati ule.
“Nawe ulisema moyoni
mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, nitakiinua kiti change juu kuliko nyota za
Mungu; name nitaketi juu ya mlima wa mkutano, katika pande za mwisho za
kaskazini. Nitapaa kupita vimo vya mawingu, nitafanana nay eye Aliye juu.
Lakini utashushwa mpaka kuzimu, mpaka pande za mwisho za shimo” Isaya 14:13-15.
“Moyo wako uliinuka
kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako;
nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama” Ezekieli
28:17
Mistari ya Biblia hiyo hapo juu unatuonesha jinsi Lucifer
ajulikanae kama ibilisi au shetani baada ya kutupwa kuzimu jinsi alivyoasi na
kutwa hadi kuzimu. Na kutupwa kwa ibilisi kuzimu haikuwa jambo rahisi, kwani
kulitokea vita kati yake na wafuasi wake dhidi ya jeshi la Malaika wa Mungu
wakiongozwa na Malaika wa vita Mikaeli.
“Na mkia wake
wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi.” Ufunuo
12:4(a). katika Biblia, kitabu hicho cha Ufunuo wa Yohana tunaoneshwa idadi
ya malaika walioasi pamoja na ibilisi, ambao kwa lugha ya ufunuo wamefananishwa
na nyota.
“Kulikuwa na vita
mbinguni, Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye
akapigana pamoja nao na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao
hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani,
aitwaye ibilisi na shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi na
malaika zake wakatupwa pamoja naye” Ufunuo 12:7-9.
Baada ya kutupwa hata kuzimu, shetani na malaika zake ambao
kwa sasa ndiyo mapepo wakaamua kutengeneza ufalme wao ujulikanao kama ‘ufalme wa
giza’ ambao unafanya kazi kinyume na “Ufalme wa Mungu”, ufalme huo wa giza
ndiyo uafalme uletao mateso hapa duniani; magonjwa, vita na hali ngumu ya
uchumi na mengine yafananayo na hayo. Ashukuriwe Mungu aliyetupa damu ya Mwana
Kondoo (Yesu Kristo) ambayo kwa hiyo tunamshinda shetani na ufalme wake wa
giza. Na ili kumshinda ni lazima kujikana, na kujikana kwenyewe ni kuamua
kumpokea Yesu Kristo kuwa mwokozi wako na kuishi maisha ya utakatifu.
“Nao wakamshinda kwa
damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao… Ufunuo 12:11”. Mstari
huo wa kitabu kitakatifu, Biblia unatufundisha ni jinsi gani tunaweza kumshinda
shetani na ufalme wake wa giza.
Baada ya shetani na ibilisi kutupwa kuzimu, ndipo Utatu
Mtakatifu wa Mungu ulipoazimia kumuumba mwanadamu. Na ile nafasi aliyokuwa nayo
sheteni katika uongozi wa Ufalme wa Mungu akakabidhiwa mwanadamu huyo. Yaani
ngazi ya pili ya ukuu; baada ya Utatu Mtakatifu wa Mungu ndipo mwanadamu huyo
anchukua nafasi akifuatiwa na malaika. Na ieleweke kwamba si kila mwanadamu anachukua
nafasi hiyo, isipokuwa ni yule tu aliyekubari kuishi kwa kuyatimiza
mapenzi ya Mungu. Ni mwanadamu au mtu yoyote aliye na Ufalme wa Mungu ndani
yake. “Na alipoulizwa na Mafarisayo,
Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, Ufalme wa Mungu hauji kwa
kuuchunguza…., Ufalme wa Mungu umo ndani yenu. Luka 17:20-21”. Na hili ni
moja ya majukumu au makusudi ya Mungu kumuumba mwanadamu, ili Ufalme wake
uwakilishwe hapa duniani kama Mbinguni. Na mwanadamu aliyemkamilifu mbele za
Mungu ndiye anayeuwakilisha Ufalme wa Mungu hapa duniani.
“Nami nikaanguka
mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi
ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa
maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii. Ufunuo 19:10”. Huyo aliyetaka
kusujudu ni Yohana Mtakatifu, na aliyetaka kumsujudia ni malaika aliyekuwa
akimuonesha maono ya Mbinguni. Malaika yule akamwambia ‘usifanye hivyo, mimi ni
mjoli wako’, maana yake yeye (malaika) ni mdogo kwake. Na aliposema ‘na wa
ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu’, alimaanisha na kila mwanadamu
aliyempokea Yesu Kristo kuwa mwokozi wake.
“Haleluya. Msifuni
Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake. Msifuni kwa
matendo yake makuu; msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. Msifuni kwa mvumo
wa baragumu; msifuni kwa kinanda na kinubi; msifuni kwa matari na kucheza;
msifuni kwa zeze na filimbi; msifuni kwa matoazi yaliayo; msifuni kwa matoazi
yavumayo sana. Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya.” Zaburi 150.
Hiyo ni sababu nyingine au makusudi ya Mungu kumuumba
mwanadamu au kumfanya mtu kwa mfano wake, mwanadamu huyu ampe Mungu sifa anazo
stahili kutoka na matendo yakemakuu yenye utukufu. Hivyo basi watu wote na tumwimbie
Mungu nyimbo za sifa na kutamka sifa midomoni mwetu kwa ajili ya Mungu wetu.
No comments:
Post a Comment