Mpendwa msomaji,
ninakusalimu kupitia Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
Nina habari njema kwako
zenye baraka kutoka kwa Mungu. Neno la Mungu linatuagiza waamini kutomuacha
elimu aende zake. Nini basi makusudi ya agizo hilo? Hakuna muamini anayeweza
kukua na kuimarisha uelewa na ufahamu wake kwa habari ya elimu ya dunia na
elimu ya Mungu pasipo kuwa na mpango madhubuti wa kuitafuta na kuikamata elimu
hiyo.
Huwezi kumtumikia Mungu
ipasavyo kama hauna elimu ya kutosha kumuhusu. Na kama haumtumikii Mungu
inavyostahili, hauwezi kukua kiroho kwa viwango vya utakatifu vinavyohitajika. Vivyo
hivyo, hauwezi kuandaa ndoa yenye upendo imara (wanaotarajia kufunga ndoa) au
kuwa na ndoa imara iliyojaa upendo, kujali na kuthamini kama hautakuwa na elimu
kuhusu ndoa kwa mujibu wa Biblia takatifu. Hauwezi kuimarisha mahusiano yako ya
ndoa au mahusiano yako na Mungu kupitia maombi peke yake, ni lazima usome.
Habari njema
ninazokuletea leo ni tarajia vitabu vizuri vyenye uwepo wa Mungu na uvuvio wa nguvu za Roho
Mtakatifu kwa Jina la Yesu Kristo.
Kitabu cha kwanza
kinaitwa, “THE HAPPIEST EVERLASTING MARRIAGE, Principles for Happiest Marriage”. Ndani ya kitabu hiki utajifunza namna ipasayo
ili kuwa na mahusiano ya ndoa imara kuanzia uchumba hadi malezi bora ya watoto
kwa kadiri utakavyo barikiwa na Mungu. Kila mmoja anakihitaji kitabu hiki, siyo
wana ndoa peke yao, hata vijana wanaotarajia kufunga ndoa miaka michache ijayo.
Kitabu cha pili
kinaitwa, “EFFECTIVE TALKING WITH GOD, Becoming God’s Friend”. Katika kitabu hiki utajifunza kukuza imani
yako na uhusiano wako na Mungu, namna sahihi ya kujihudhurisha mbele za Mungu
na kufikia viwango vya kuwa rafiki wa Mungu.
Vitabu hivi bado
havijawa tayari kwa sasa, vipo katika hatua ya “peer reviewing” ili kuhakiki
ubora wake. Miezi michache ijayo, vitabu vyote vitakuwa vinapatikana sokoni na
vitauzwa na wauzaji wa kimataifa kwa njia ya mtandao kama Amazon.com. Vitabu vyote
vimeandikwa kwa lugha ya Kiingereza ili kuvipa wigo mkubwa zaidi wa wasomaji
kwa Jina la Yesu Kristo.
Usipange kuvikosa
vitabu hivi, na Mungu atakubariki sana. Amina.
No comments:
Post a Comment