Kuna
tofauti kubwa kati ya toba na toba ya kweli, toba haimalizi kosa/dhambi lakini
toba ya kweli inamaliza kosa/dhambi. Na baada ya toba ya kweli, Mungu huzifuta
dhambi zetu zote (Isaya 43:25). Unapoamua kufanya toba, fanya toba ya kweli
maana hiyo ndiyo toba yenye msamaha wa dhambi ndani yake.
Toba na
toba ya kweli zina sifa kadhaa zinazofanana; kutambua kosa/dhambi, kulijutia na
kuliombea msamaha.
Tofauti ya
toba na toba ya kweli ni kuacha kuitenda tena dhambi uliyokwisha kuiombea
msamaha, hii ndiyo toba anayoipenda na kuitaka Mungu.
TOBA.
Mathayo
27:3, 5 “Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona amekwisha kuhukumiwa,
alijuta akawarudishia wakuu wa makuhani na wazee vile vipande thelathini vya
fedha, akasema, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia. Akavitupa vile
vipande vya fedha katika hekalu, akaondoka; akaenda, akajinyonga”.
Toba ni
kulitambua kosa, kulijutia na kuliombea msamaha. Muomba toba anaweza akayarudia
makosa au anaweza akalitambua kosa na akalijutia lakini asiliombee msamaha. Na jinsi
unavyorudia kosa au unafanya kosa, unalijutia lakini hauliombei msamaha ndivyo
hofu ya Mungu inavyozidi kuondoka ndani yako na dhamira ya kukufanya uitambue
dhambi na kuijutia nayo inatoweka. Mtu wa namna hii anafikia mahali anakufa
kiroho, na mfu wa roho ni kazi sana kumrudia Mungu. Mtu huyu anahitaji huduma
ya ukombozi yenye neema ya Mungu mwenyewe. (Luka 11:24-26).
Shetani ndiye
anayewadanganya watu kwamba wametenda dhambi kubwa sana zisizo na msamaha, na
hata kuiua dhamira iliyo ndani ya mtu ili mtu huyo asitafute toba ya kweli.
TOBA YA
KWELI.
Luka
15:11-19 “. . . nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba,
nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu
ya mbingu na mbele yako. Lakini baba aliwaambia watumwa wake, lileteni upesi
vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni; kwa kuwa
huyu mwanangu alikuwa amekufa naye amefufuka, alikuwa amepotea naye ameonekana.”
Toba ya kweli
ni kulitambua kosa, kulijutia, kuliombea msamaha na kutolitenda tena. Toba ya
kweli urudisha utukufu na hofu ya Mungu kwako. Ili usirudie tena dhambi
uliyokwisha iombea msamaha unapaswa kujikita katika maombi na kuepukana na
mazingira yasababishayo dhambi hiyo. (Zaburi 1:1-2 na Waefeso 4:28).
Hakuna dhambi
isiyo na msamaha kwa Mungu, dhambi zote zinasamehewa kwa sababu neema na rehema
za Mungu ni juu ya wanadamu wote, wote tunaweza kusamehewa ikiwa tutafanya toba
ya kweli. (Zaburi 103:11-13 na 2 Wakorintho 5:17).
Unataka kumpokea Yesu Kristo leo? Bonyeza hapa.
No comments:
Post a Comment