1 WAKORINTHO 15:1-2
BASI NDUGU ZANGU NAWAARIFU ILE INJILI NILIYOWAARIFU,
AMBAYO NDIYO MLIYOIPOKEA, NA KATIKA HIYO MNASIMAMA, NA KWA HIYO MNAOKOLEWA:
IKIWA MNAYASHIKA SANA MANENO NILIYOWAHUBIRI; ISIPOKUWA MLIAMINI BURE.
Neno la Mungu (hapo juu) linatuambia habari ya
injili ambayo kwa hiyo tunapokea zawadi au neema ya kuokolewa na kupokea uzima
wa milele. Injili ya YESU KRISTO ambayo ndani yake kuna nguvu ya kutuokoa.
Ili upokee wokovu ni lazima uisikie injili ya Yesu
Kristo na habari ya Ufalme wa Mungu Baba, pasipo injili ya Yesu Kristo hakuna
wokovu, injili ya Yesu Kristo pekee!
Matendo ya mitume 10:3-6.
Kornelio, mtu mtauwa (hajaokoka bado) anatokewa na
malaika katika maono, anaambiwa atume mtu kwa Simoni Petro, aje nyumbani mwake
amwambie yampasayo kutenda….
Matendo ya mitume 11:14
Malaika yule anamwambia Kornelio amwite Simoni Petro
aje amwambie maneno au habari itakayomwokoa… injili ya Yesu Kristo!
Matendo ya mitume 16:30-32
Baada ya milango ya milango ya gereza kufunguka, na
mlinzi wa gereza kutaka kujiua Paulo na Sila wakamzuia. Wakamwambia habari
njema ya Yesu Kristo… injili ya Yesu Kristo! Wakamwambia mwamini Bwana Yesu
nawe utaokoka, wakamwambia neno la Bwana (Yesu), yeye na nyumba yake yote,
wakaokoka.
Mathayo 24:14 na Marko 13:10.
Neno la Mungu linazidi kututhibitishia kuwa hakuna
wokovu pasipo injili ya Yesu Kristo na Ufalme wa Mungu. Injili inahubiriwa na
itahubiriwa ulimwenguni kote ili wewe ambaye bado hujampokea Yesu Kristo na
hujaokoka upate nafasi ya kupokea zawadi hiyo.
Baada ya kuisikia injili ya Yesu Kristo na kuokoka
ni lazima uishi maisha ya kudumu na kutekeleza kinachokuambia katika injili ya
Yesu Kristo. Kuishi maisha tofauti na injili ya wokovu ni kazi bure, ni
kupoteza muda. IKIWA UNAISHIKA SANA INJILI ULIYOHUBIRIWA NA UNAYOHUBIRIWA,
UTAPOKEA UZIMA WA MILELE.
2 Yohana 1:9
Mungu anakuambia, usipodumu kufuata, kutenda na
kuishi mafundisho ya injili ya Yesu Kristo, hauna Mungu. Wokovu ulioupokea,
pasipo kuishi ikuelekezavyo injili ya Kristo, ni ubatili mtupu na kujilisha
upepo.
Luka 6:46.
Yesu Kristo anakuhoji, kwanini unajiita umeokoka,
mkristo, unaimba kwaya, wewe ni kiongozi na unahudhuria ibada lakini hauyatendi
anayokuelekeza katika injili yake?
Ikiwa unaisikia na kuisoma injili ya Yesu na
hujaokoka bado, ni lazima uamue leo kumpokea Yesu Kristo na uyakabidhi maisha
yako kwake, uokoke.
Na ikiwa wewe ni mkristo, lakini unatenda kinyume na
injili ya Yesu Kristo, ni lazima ubadilike sasa. Neno la mungu linakuambia,
kuishi kinyume na injili ni bure, imani yako ni bure!
BONYEZA HAPA: Uokoke.
No comments:
Post a Comment