Monday, July 15, 2013

HII SI YA KUKOSA!!!

Nakusalimu kwa Jina la Yesu Kristo!

Natumaini u mzima wa afya, kama mimi nilivyo mzima pia, shukrani zimrudie Mungu mwenyewe anayetupa uhai bure.

Kuanzia jumapili ya tarehe 21/07/2013, tutaanza somo jingine lenye kichwa kisemacho;

"UNAWEZA KUWA UNAISHI NA LAANA PASIPO WEWE MWENYEWE KUJUA"

ni somo zuri sana, lenye pumzi ya Mungu. na kupitia somo hilo, Mungu anakwenda kukutoa mahali ulipo ambapo haustahili kuwepo na anakuinua na kukuketisha meza moja na wafalme, kwa kifupi utakwenda kuziona baraka za Mungu zakianza kufuatana na wewe kwani laana na mikosi yote inakwenda kuvunjwa na wewe kuwekwa huru, katika jina la Yesu Kristo, Amina.

Katika somo hilo tutakwenda kuangalia kwa undani zaidi mambo yafuatayo:-

  1. maana ya laana
  2. laana inaletwa/sababishwa na nani?
  3. kwanini ulaaniwe?
  4. vitu gani vinaweza kulaaniwa katika maisha yako?
  5. je unaweza kuwa umelaaniwa pasipo wewe mwenyewe kujua?
  6. kuvunja laana na mikosi kwa Jina la Yesu Kristo.
Hivyo basi usithubutu kulikosa somo hili, mtaarifu na mwenzako ili Mungu akubariki sana kwa kushiriki katika kuutangaza ufalme wake.

1 comment:

Featured Post

MARRIAGE: DEFINITION, ORIGIN, PURPOSE AND HAPPINESS

Dear brother/sister, greetings in the name of Jesus Christ. Today I want to share with you a very minor part of our powerful, lovely an...

Popular Posts